Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ASEC yaishushia mvua ya magoli Jwaneng Galaxy

Asec Yashinda.webp ASEC yaishushia mvua ya magoli Jwaneng Galaxy

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Simba SC, Kundi B linazidi kunoga, baada ya Mnyama kujinyakulia alama tatu leo Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar, waliokuwa wanaongoza kundi hilo, ASEC Mimosas wamezidi kujikita kileleni kwa kuwakanda Jwaneng Galaxy 3-0.

ASEC walikuwa nyumbani leo kuwakaribisha Jwaneng ambao walikuwa na alama zao 4, sasa wamebaki nazo hizo na ASEC sasa wanaongoza kundi wakiwa na alama 10.

Nafasi ya pili sasa ni mali ya Simba yenye alama 5, Jwaneng ya tatu yenye alama 4 na anayeshika mkia ni Wydad Casablanca ambaye ana alama 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live