Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AS Vita waelekea Dar kuweka kambi ya siku 14

As Vita Ers.jpeg AS Vita waelekea Dar kuweka kambi ya siku 14

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha AS Vita ya DR Congo kipo njiani kuja nchini Tanzania kuweka kambi ya siku 14 kujiandaa na msimu mpya.

Vita wakiwa hapa wanataka kuweka kambi yao jijini Dar es Salaam ikiwa ni ushauri wa kocha wao msaidizi Raul Shungu.

Shungu aliwahi kufanya kazi nchini miaka ya nyuma akiifundisha Yanga kwa mafanikio kwa kutwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kikosi hicho kinachofundishwa na kocha Mfaransa Dominique Cionci pia kimepanga kucheza mechi kadhaa za kirafiki hapa nchini.

Bado haijafahamika endapo kama kitacheza na miamba ya soka Tanzania Yanga, Simba au Azam katika ratiba yao hiyo.

"Tunakuja Tanzania tutaweka kambi hapo kujiandaa na msimu mpya, tumeona tuje Tanzania hasa hapo Dar es Salaam kuna viwanja vizuri, tutaangalia kama tutapata kucheza mechi na timu za hapo hizi kubwa," amesema Shungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live