Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

APR wangeongeza utulivu, Yanga wangefungwa 5 : Master Tindwa

Yanga V APR APR wangeongeza utulivu, Yanga wangefungwa 5 : Master Tindwa

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Master Tindwa anasema laiti APR wangeongeza utulivu kwenye mechi yao dhidi ya Yanga SC, wangeweza kuwafunga Mbingwa hao watetezi wa Kombe la NBC goli 5.

Yanga alifurushwa kwenye mashindano hayo ya Mapinduzi baada ya kufungwa 3-1 na APR jana Januari 7, 2024 katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

"Kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri, Yanga walicheza kawaida ila walikutana na timu ya kawaida wakaifunga magoli matano, mchezo dhidi ya Jamus walipata shida kupata ushindi na ushindi ulikuja dakika za lala salama.

Jana dhidi ya APR ilikuwa moja kati ya mechi nzuri na wamefungwa magoli matatu.

Kipindi cha kwanza Yanga walitawala na waliona game kama rahisi, back pass zilikuwa nyingi hata sehemu ambazo hazikuwa na ulazima."

Goli la kusawazisha la APR ndio liliwarudhisha mchezoni na kama wangekuwa na utulivu zaidi ule mnara wa 5G ungesimama jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live