Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFRICAN FOOTBALL LEAGUE: Enyimba vs Wydad vita ya wakubwa

Enyimbaaaaaaa AFRICAN FOOTBALL LEAGUE: Enyimba vs Wydad vita ya wakubwa

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ndio, michuano ya African Fooball League inafunguliwa rasmi kwenye ardhi ya Tanzania pale Uwanja wa Benjamin Mkapa leo.

Baada ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly michezo mingine pia itafuata ambapo Enyimba ya Nigeria itacheza na Wydad Casablanca ya Morocco.

Timu hizi mbili zitaanza kukutana Oktoba 22, kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio International Stadium huko Uyo, Nigeria na marudiano yatakuwa pale Stade Mohammed V nchini Morocco na kwa mechi ya mkondo wa kwanza mwamuzi atakayesimama kati kati ni Alhadi Allaou Mahamat raia wa Chad.

Hapa tunekuleta rekodi na historia ya timu zote kuanzia zilipoanzishwa hadi sasa.

ENYIMBA

Hii ndio timu yenye mafanikio zaidi nchini Nigeria. Wababe hawa ndio wanaongoza kwa kuchukua taji la Ligi Kuu nchini humo mara nyingi zaidi tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu nchini humo mwaka 1972.

Enyimba imechukua taji hilo mara tisa, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2001 na ikafanya hivyo msimu uliopita pia.

Timu ambayo imeanzishwa mwaka 1976, kwa sasa inaongozwa na lejendi wa Nigeria ambaye ni mchezaji wa zamani wa Arsenal, Ajax na Inter Milan Nwanko Kanu, anayehudumu kama mwenyekiti, huku wamiliki wakiwa ni serikali ya Mji wa Abia.

Ukiondoa ubabe wake kwenye ligi ya ndani, Enyimba pia ina rekodi za kipekee kwenye michuano ya Kimataifa.

Kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa, ukiondoa msimu huu ambapo wametolewa na Al Ahly Benghazi, huko nyuma walishiriki jumla ya mara nane.

Kati ya hizo ilifanikiwa kuchukua ubingwa mara mbili mwaka 2003 ambapo ilicheza fainali dhidi ya Ismaily ya Misri, mchezo wa kwanza pale Enyimba International Stadium iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na fainali ya pili pale nchini Misri kwenye dimba la Ismailia ikafungwa bao 1-0. Msimu huo kwenye hatua ya makundi ilikuwa kundi moja na Simba ambayo ilimaliza nafasi ya tatu kwa alama saba wakati Enyimba ikiwa kinara.

Ilichukua tena ubingwa wa pili mfululizo mwaka 2004 na wakati huu ilikutana na Etoile du Sahel ambapo kwenye mchezo wa kwanza pale Nigeria ilishinda mabao 2-1 na marudiano kule Tunisia ikafungwa mabao 2-1. Baada ya hapo ikaenda kuchukua ubingwa kwa penalti ikipata penalti 5-3.

Mbali ya kuchukua ubingwa Enyimba imetinga hatua ya makundi mara tatu mwaka 2006, 2008 na 2016, pia imecheza nusu fainali mbili mwaka 2008 na 2011.

Kwenye Kombe la Shirikisho imeshiriki mara nne na mafanikio makubwa iliyoyapata huko ni kucheza nusu fainali mara moja mwaka 2018 sambamba na robo fainali mara mbili mwaka 2020 na 2021. Mara moja iliishia hatua ya 16 bora ambayo ni mwaka 2010.

Enyimba pia ina makombe mawili ya CAF Super Cup, la kwanza ikichukua mwaka 2004 ilipocheza dhidi ya Etoile Sportive du Sahel iliposhinda bao 1-0, pia ikachukua mwaka 2005 ilipocheza dhidi ya Hearts of Oak ya Ghana ambapo ilishinda mabao 2-0.

WYDAD CASABLANCA

Unaweza ukaiita miamba ya soka ndani ya Afrika, ukiiondoa Al Ahly, moja ya timu ambazo zimekuwa na rekodi nzuri kwenye michuano ya kimataifa ni hii.

Timu hii ambayo ni mali ya wanachama ina makazi yake katika Jiji la Casablanca nchini Morocco.

Hii ndio timu inayoongoza kupata mafanikio ndani ya Morocco ikiwa imechukua jumla ya mataji 22 ya Ligi Kuu nchini humo, ikifuatiwa na As Far ambayo imeshinda mataji 22, tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo mwaka 1905.

Mbali ya kuwa mabingwa hii ndio timu iliyomaliza nafasi ya pili ya ligi hii mara nyingi zaidi ikifanya hivyo mara 13.

Kwenye michuano ya kimataifa Wydad imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu katika misimu 16 iliyoshiriki, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1992 ilipocheza na Al Hilal ya Sudan ambapo mchezo wa kwanza pale Stade Mohamed V, Casablanca iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na mchezo wa marudio kule l-Hilal Stadium, Omdurman nchini Sudan ikatoka sare ya bila kufungana.

Ubingwa wa pili iliupata kwenye michuano ya mwaka 2017 ambapo ilicheza dhidi ya Al Ahly, mechi ya kwanza pale Misri ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na mchezo wa marudiano Morocco Wydad ilishinda bao 1-0. La tatu wakalitwaa hivi karibuni pale Stade Mohamed V.

Chanzo: Mwanaspoti