Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFL hii ndio bora kuliko ijayo itakayokuwa na washiriki wengi - Ahmed Ally

AFL Hii Ndio Bora Kuliko Ijayo Itakayokuwa Na Washiriki Wengi   Ahmed Ally.jpeg AFL hii ndio bora kuliko ijayo itakayokuwa na washiriki wengi - Ahmed Ally

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Shindano la Africa Footbal League (AFL) la mwaka huu ndio lina hadhi kubwa kuliko litakalofanyika misimu inayofata.

Ahmed ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2023 alipokuwa akifanya hamasa za kuelekea kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa Ijumaa hii Oktoba 2023 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Maandalizi haya babkubwa yanayofanyika yanatuhitaji kwenda uwanjani. Hakuna Mwanasimba anatakiwa kubaki nyumbani, hiyo siku ni kwenda uwanjani. Historia hiyo itabaki kwa vizazi na vizazi."

"Lazima tuambiane ukweli AFL ya safari hii imeshirikisha timu nane bora na Mnyama yupo kati ya timu hizo bora, AFL zijazo zitakusanya kila mtu ambayo haitakuwa na thamani sawa na hii ya kwanza."- Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live