Mashabiki wengi wanaoendelea kumiminika katika uwanja wa Benjamin Mkapa wamekutana na kitu cha tofauti kama walivyozoea.
Leo Simba inashuka kumenyana na Al Ahly saa 12:00 jioni mchezo wa ufunguzi wa African Football League ambao unashirikisha timu nane bora Barani Afrika. Iko hivi mashabiki wakifika katika mageti ya kuingia uwanjani wanatakiwa kuacha chupa zao za maji ya kunywa getini tofauti na ilivyozoeleka katka michezo mingi iliyopita.
Imekuwa jambo la kushtua lakini wameelewa baada ya kupewa maelekezo na polisi waliosimama vyema kuimalisha ulinzi wa raia na mali zao.
Hakuna aliyebisha baada ya kuambiwa kufanya hivyo walitekeleza na kuingia ndani kwa utaratibu mzuri.