Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFL: Imeisha hiyo, bao la ugenini lipo kama kawa!

Simba Vs Ahly Vikosi Kanuni za African Football League.

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumeibuka maswali kuelekea michezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya kombe la Afrika (AFL) kesho kati ya Simba SC dhidi ya wenyeji Al Ahly, katika dimba la Cairo baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya bao 2-2 juzi katika Dimba la Mkapa.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya African Football League kuelekea mchezo wa kesho kati ya Al Ahly dhidi ya Simba lile bao la ugenini lipo.

Kanuni ya 15 kifungu kidogo cha tatu kimeondoa sintofahamu hiyo ikiweka wazi kwamba kwa mechi za hatua ya robo fainali, nusu fainali timu itakayokuwa na idadi kubwa ya mabao ya ugenini itafuzu hatua inayofuata.

Kanuni hiyo hiyo kipengele kinachofuata ikaeleza kuwa bao hilo la ugenini linatumika mpaka kwenye mchezo wa fainali ambapo timu yenye mabao mengi baada ya mechi ya pili itachukua ubingwa.

Kwa upande wa kanuni ya 16 kipengele cha kwanza nacho kimeeleza kuwa kuanzia hatua ya robo fainali endapo timu zote zitalingana kwa mabao ya kufunga na yale ya ugenini mechi hiyo itaamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Ufafanuzi huo unaifanya Simba kesho kuendelea kuupigania ushindi kwenye mchezo huo wa ugenini au sare ya mabao 3-3 na zaidi ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali.

Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 hapa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Ahly ambao ni mabingwa wa Afrika na kesho saa 11 jioni timu hizo zitamalizana kwa mchezo wa pili wamarudiano utakaopigwa Jijini Cairo nchini Misri.

Kanuni hiyo inaeleza kuwa, timu yenye idadi kubwa ya mabao ya kufunga ya ugenini itakwenda hatua inayofuata, (Kwa kesi ya Simba) Kama Simba itaenda sare ya 1-1 au Suluhu (0-0) basi Al Ahly itakwenda nusu fainali.

Endapo Simba itapata Sare ya 2-2 basi mchezo utakwenda kwenye Changamoto ya mikwaju ya Penalt na mwishowe Endapo Simba itapata Sare ya 3-3 au zaidi ya hapo itakwenda Nusu fainali.

Kwa hiyo, endapo Simba au Al Ahly itashinda matokeo ya Ushindi kwenye mechi basi hakuna mjadala mwenye matokeo bora ya wingi wa mabao ya kufunga atatinga Nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live