Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON yaota mbawa kwa Miquissone

Jose Luis Miquissone Kabini Jose Luis Miquissone

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Msumbiji imetaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 watakaoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 mwakani huko Ivory Coast, huku jina la winga wa Simba, Luis Miquissone likikosekana.

Miquissone alikuwa miongoni mwa nyota 50 walioitwa na Kocha Chiquinho Conde katika kikosi cha awali cha Msumbiji lakini ameshindwa kupenya katika majina 23 ambayo yataipeperusha bendera ya taifa hilo huko Ivory Coast.

Mkongwe Elias Domingues Pelembe mwenye umri wa miaka 40 akiitumikia UD Songo kwa sasa ataendelea kuwa nahodha wa kikosi cha Msumbiji 'Mambas' kwenye Afcon mwakani ambacho kinaundwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa ndani ya Msumbiji.

Nyota wa Atletico Madrid, Reinildo Mandava anabeba matumaini ya Msumbiji katika mashindano hayo kama ilivyo kwa Geny Catano wa Sporting Lisbon.

KIKOSI KAMILI

Makipa: Maria Joao, Ivane Urrubal na Ernan Siluane huku

Mabeki: Edmilson Dove, David Malembana, Bruno Langa, Domingos Macandza, Infren Matola, Reinildo Mandava, Edson Sitoe na Feliciano Jone.

Viungo: Amade Momade, Joao Bonde, Ricardo Guimares, Shaquille Nangy na Alfons Amade wakati

Washambuliaji: Pelembe, Clesio Bauque, Geny Catamo, Witiness Quembo, Gildo Vilanculos, Stanley Ratifo na Lau King.

Chanzo: Mwanaspoti