Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON yampa ulaji Kipa Nigeria

Stanley Nwabali Ulaji Mlinda mlango wa timu ya taifa Nigeria ‘Super Eagles’ Stanley Nwabali

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa timu ya taifa Nigeria ‘Super Eagles’ Stanley Nwabali (27) ameanza kutamaniwa katika ligi za Saudia Arabia na Uingereza.

Nwabali amefanya vyema katika Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) yaliyofanyika nchini Ivory Coast na taifa hilo likabakiza kombe hilo nyumbani kwa kuifunga Nigeria ya Nwabali.

Kipa huyo anayekipiga Chippa United ya Afrika Kusini huenda akaondoka klabuni hapo itakapofika usajili wa majira ya joto baadae.

Klabu ya Queens Park Rangers ya England ( Daraja la Pili ) na El Ittifaq ya Saudi Arabia zipo mstari wa mbele kuiwania saini ya kipa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live