Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON imetufunza kuliheshimu soka

Ziyech XHakimi X Amrabat AFCON imetufunza kuliheshimu soka

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Soka ni mchezo wa kushangaza kwani umekuwa na matokeo ambayo wakati mwingine yanakuwa hayakutegemewa kama yanaweza kutokea au hayatatokea.

Ukifuatilia kinachoendelea kwenye fainali za Afcon mwaka huu huko Ivory Coast hapana shaka utazidi kuona upekee wa mchezo huo, kwani mengi ambayo yalitarajiwa yamekuwa yakienda kinyume na kumekuwa na matokeo ya kushangaza.

Kwanza kuna timu ambazo zilikuwa hazipewi nafasi kubwa ya kutamba kwenye mashindano hayo zimeonekana kufanya vyema na kugeuka kuwa tishio kiasi ambacho baadhi zimeanza kupewa nafasi kubwa ya kufika hatua za juu za kwenye fainali hizo.

Mfano ni timu ya taifa ya Cape Verde ambayo haikuonekana kama ingeweza kutamba katika kundi B lililokuwa na timu za Ghana, Misri na Msumbiji lakini ikaweza kuwa kinara kwa kutopoteza hata mechi moja kwenye kundi na sasa ipo katika hatua ya robo fainali.

Halafu kuna hili la kufanya vibaya kwa timu nyingi ambazo zilipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ambapo zimejikuta zikiaga kabla hata ya nusu fainali kwa kuishia ama kwenye makundi au hatua ya 16 bora.

Hapa unavyosoma habari hii, timu inayotajwa kuwa bora zaidi Afrika kwa sasa, Morocco, waliokuwa mabingwa watetezi wa Afcon, Senegal, Misri ambayo ilifika fainali katika awamu iliyopita, Algeria, Ghana, Tunisia na Cameroon zote zinatazama mechi kupitia runinga baada ya kutolewa.

Halafu kuna yale matokeo ya kushangaza ambayo baadhi ya timu zilifungwa na wapinzani ambao hawakuonekana kuwa tishio huku baadhi ya timu zilizopenya kama ‘Best Losers’ kutoboa katika mechi za hatua ya 16.

Somo tunalolipata hapa ni kwamba mchezo wa soka pasipo kujali unakutana na nani au unashiriki mashindano gani, unahitaji maandalizi ya kina ya kiufundi na yale yasiyo ya kiufundi ili kuifanya timu iwe na utayari wa kushindana.

Hizo timu ambazo hazikutegemewa na zimefanya vizuri hilo halijatokea kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya maandalizi ambayo zilifanya kabla ya kuanza kwa fainali za Afcon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live