Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON U-17: Filimbi itapulizwa Taifa na Azam Complex

51075 PIC+FILIMBI

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Michezo 16 itapigwa kwenye Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 ‘Afcon 17’ ambayo itachezwa kwenye viwanja viwili ambavyo ni Uwanja wa taifa na Azam Complex vya jijini Dar es Salaam.

Hii itakuwa awamu ya 13 kufanyika kwa Afcon U17 tangu kuanzishwa kwake 1995 pia itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali hizo.

Fainali hizo zinashirikisha mataifa nane kutoka ya Afrika akiwemo mwenyeji, timu hizo zimegawanywa kwenye makundi mawili A na B na kila kundi limeundwa na timu nne.

Timu za Kundi A ni Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda katika kundi hilo itapigwa michezo sita ambayo itaamua timu mbili zitakazosonga kwenda nusu fainali.

Serengeti Boys vs Nigeria U17

Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo Jumapili ya Aprili 14, Serengeti Boys itakuwa na kibarua cha kupepetana na timu ya taifa la Nigeria mpambano utakaoanza saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Angola vs Uganda

Baada ya kumalizika mchezo kati ya Serengeti Boys na Nigeria U17, kutafuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo A kati ya vijana wa Angola na Uganda kwenye uwanja huo huo wa taifa, Saa 1:00 usiku.

Nigeria vs Angola

Michezo ya pili kwa timu za kundi hili itaendelea kupigwa Aprili 17 kwa vijana wa Nigeria kucheza na Angola, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioni.

Uganda 17 vs Serengeti Boys

Majira ya saa moja usiku, Serengeti Boys watacheza mchezo wao wa pili dhidi ya Uganda kwenye uwanja huo huo wa taifa baada ya kumalizika kwa mechi ya vijana wa Nigeria dhidi ya Angola.

Serengeti Boys vs Angola U17

Serengeti Boys watamaliza michezo yao ya makundi kwa kucheza na vijana wenzao wa Angola, Aprili 20, saa 10:00 jioni , Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nigeria vs Uganda

Wakati Serengeti Boys watakapokuwa wanamalizana na Angola, muda huo huo vijana wa Nigeria na Uganda nao watakuwa wanacheza mchezo wao wa mwisho kwenye kundi hilo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje ya jiji la Dar es Salaam.

Kundi B lenyewe ni Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal wao nao watakuwa na michezo sita kwenye kundi lao kabla hatua ya nusu fainali ambayo itakuwa na michezo miwili, mshindi wa tatu mmoja pamoja na fainali.

Guinea vs Cameroon

Mchezo wa kwanza Kundi B utachezwa Aprili 15 kati ya timu ya vijana ya Guinea na Cameroon ambao utaanza saa 10:00 jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Morocco vs Senegal

Vijana wa miamba ya soka la Afrika, Morocco na Senegal wao wataonyeshana umwamba saa moja usiku, Aprili 15 baada ya kumalizika mchezo kati ya vijana wa Guinea na Cameroon.

Michezo mingine

Aprili 18-

Cameroon vs Morocco,

Azam Complex (saa 10:00 jioni)

Aprili 18-

Senegal vs Guinea, Azam

Complex (saa 1:00 usiku)

Aprili 21-

Guinea vs Morocco,

Uwanja wa Taifa (saa 10:00 jioni)

Aprili 21-

Cameroon vs Senegal,

Azam Complex (saa 10:00 jioni)



Chanzo: mwananchi.co.tz