Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON 2023 itakavyopunguza utamu Ligi Kuu England

Onana Salah Fdb AFCON 2023 itakavyopunguza utamu Ligi Kuu England

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikikimikiki ya mchezo wa soka ya kusaka ubingwa wa Afrika, (Afcon 2023) inatarajia kuanza mapema mwezi ujao huku Ligi Kuu England ikitarajiwa kuathirika kwa kiasi kubwa kutokana na mastaa wengi kwenda kukipiga kwenye michuano hiyo.

Supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah anatarajiwa kwenda kuwa nahodha wa Misri kwenye fainali hizo za Afcon 2023 zitakazofanyika Ivory Coast, akiwa ni mmoja kwenye orodha ya mastaa kibao watakaorejea Afrika kuzichezea timu zao za taifa.

Makala haya yanahusu mastaa wa Ligi Kuu England ambao watazipa kisogo timu zao za klabu kwa kipindi cha mwezi mmoja kwenda kuzitumikia timu zao za taifa za Afrika kwenye Afcon 2023.

Mastaa wenyewe

Arsenal: Mohamed Elneny (Misri), Thomas Partey (Ghana)

Aston Villa: Bertrand Traore (Burkina Faso).

Bournemouth: Dango Ouattara (Burkina Faso), Antoine Semenyo (Ghana), Hamed Traore (Ivory Coast).

Brighton: Simon Adingra (Ivory Coast), Tariq Lamptey (Ghana), Samy Chouchane (Tunisia).

Brentford: Yoane Wissa (DR Congo), Bryan Mbeumo (Cameroon), Frank Onyeka (Nigeria).

Burnley: Anass Zaroury (Morocco), Lyle Foster (Afrika Kusini).

Chelsea: Nicolas Jackson (Senegal).

Crystal Palace: Cheick Doucoure (Mali), Jordan Ayew (Ghana), Jeffrey Schlupp (Ghana).

Everton: Abdoulaye Doucoure (Mali), Idrissa Gueye (Senegal).

Fulham: Calvin Bassey (Nigeria), Alex Iwobi (Nigeria).

Liverpool: Joel Matip (Cameroon), Mohamed Salah (Misri).

Luton Town: Issa Kabore (Burkina Faso), Pelly Ruddock Mpanzu (DR Congo).

Man City: Haina mchezaji yeyote kwenye Afcon 2023.

Man United: Andre Onana (Cameroon), Amad Diallo (Ivory Coast), Sofyan Amrabat (Morocco), Hannibal Mejbri (Tunisia).

Newcastle: Haina mchezaji yeyote kwenye Afcon 2023.

Nottingham Forest: Serge Aurier (Ivory Coast), Willy Boly (Ivory Coast), Ibrahim Sangare (Ivory Coast), Cheikhou Kouyate (Senegal), Moussa Niakhate (Senegal), Ola Aina (Nigeria), Emmanuel Dennis (Nigeria), Taiwo Awoniyi (Nigeria).

Sheffield United: Benie Traore (Ivory Coast) Ismaila Coulibaly (Mali) Anis Ben Slimane (Tunisia).

Tottenham: Pape Matar Sarr (Senegal) Yves Bissouma (Mali).

West Ham: Said Benrahma (Algeria) Mohamed Kudus (Ghana) Maxwell Cornet (Ivory Coast) Nayef Aguerd (Morocco).

Wolves: Rayan Ait-Nouri (Algeria) Boubacar Traore (Mali).

KIPUTE NI LINI?

Afcon 2023 itafanyika mwaka 2024, licha ya jina lake kuandikwa tofauti. Michuano hiyo awali ilipangwa kufanyika mwaka jana, lakini ilishindikana. Afcon itaanza rasmi Januari 13, kwa mechi ya wenyeji Ivory Coast dhidi ya Guinea-Bissau na kumalizika Februari 11. Hatua ya makundi itakamilika Januari 24.

MECHI GANI ZA LIGI WATAZIKOSA

Wachezaji wote watakaokwenda kwenye Afcon 2023 watazikosa mechi za Ligi Kuu England za kuanzia wiki ya 21 na hiyo itakwenda kwa wikiendi mbili zaidi.

Kwa wachezaji ambao timu zao zitakomea kwenye hatua ya makundi, wanaweza kukosa mzunguko mmoja tu wa mechi za EPL, lakini kwa watakaobahatika kufika fainali, watakosa hadi wiki nne za mikikimikiki hiyo ya kibabe kabisa ya Ligi Kuu England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live