Timu ya taifa ya Tanzania imepata Sh l.2 bilioni za Kitanzania baada ya kumaliza hatua ya makundi ya fainali za AFCON 2023 ikiwa nafasi ya nne.
Stars ambayo haikupata ushindi kwenye kundi F ambalo ilikuwa na Morocco, DR Congo na Zambia, iliambulia sare mbili tu ilizopata mbele ya Congo na Zambia.
Kiasi hicho cha pesa ni zawadi inayopata timu ya mwisho ya Kundi kwa mujibu wa tovuti rasmi ya CAF huku timu zilizomaliza nafasi ya tatu zinapata Sh l.7 bilioni na zile zilizofuzu kwenda hatua ya l6 bora zimepata bilioni 2.
Stars ilikusanya Pointi hizo mbili kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia pia sare ya bila kufungana mbele ya DR Congo ambayo ilicheza nayo kweye mechi ya mwisho ya kundi.
Mwaka huu CAF imeongeza zawadi ambapo mshindi atapata Dola 7 milioni (Sh 17.7 bilioni) ikiwa ni ongezeko la Dola 2 milioni kutoka Dola 5 milioni ilizopewa Senegal kwa ubingwa wa 2021.