Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON 2023: TFF yaitwa Kamati ya Olimpiki

Afcon Trophy Cs2zw7ey9qbi1i0e971ya3tcx 660x400 AFCON 2023: TFF yaitwa Kamati ya Olimpiki

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania ‘TOC’, Henry Tandau ameliita Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ mezani kuelekea maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ itakayoandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.

Safari ya timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ivory Coast ilifikia tamati juzi Jumatano (Januari 24) baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kushika mkia kwenye Kundi F ikiwa na pointi mbili.

Tandau akizungumza jijini Dar es salaam amesema fainali za Ivory Coast kwa Taifa Stars zimefikia tamati na muhimu kwa TFF kuona namna gani wanajiandaa kwa mashindano hayo ambayo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

“Sisi kama Kamati ya Olimpiki tuko tayari kushirikiana na TFF kama wadau muhimu kuelekea michuano ya Kombe la Fainali ya Mataifa ya Afrika ambayo Tanzania tutaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live