Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON 2022 yaongeza hofu Ulaya, Wachezaji kuondoka

Afcon 2022 Michuano ya AFCON itafanyika Januari 2022

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Klabu Ulaya (ECA) kimeonyesha hofu yake juu ya wachezaji wa Afrika ambao watashiriki michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika (AFCON 2022) ambayo inategemea kuanza kutimua vumbi Cameroon Januari 9 – Februari 6.

Hofu ya kwanza kwa ECA ni juu ya uwezekano wa kuwapa kwa haraka wachezaji hao baada ya kumalizika kwa michuano hiyo kwani taifa kama England limeweka vizuizi vya baadhi ya mataifa ya Afrika kuingia nchini humo ikiwa ni sehemu ya kupambana na wimbi jipya la Covid-19. Hivyo michuano inaweza kumalizika lakini wachezaji wasiruhusiwe kucheza wakiwa kwenye kujitenga mwenyewe (isolation time).

Jambo lingine ambalo ECA wanalitazama ni uwezekano wa kushuka daraja la ubora kwa klabu ambazo wachezaji wa Afrika wamekuwa wakisimama kidete katika mafanikio yao mathalani Liverpool yenye Mohammed Salah na Sadio Mane.

Kutokana na hofu hiyo, ECA wamefikisha maoni yao katika Shirikisho la Kandanda Duniani Fifa kuona namna ambavyo fainali za Afcon 2022 zitafanyika bila kuathiri shughuli za kimichezo Ulaya.

Kama mapendekezo yao yatapewa uzito na FIFA inawezekana baadhi ya wachezaji wakazuiliwa kwenda kwenye michuano hiyo, hii inakumbusha tukio la vilabu vya England vilikataa kuwaachia wachezaji wake kwenda kwenye majukumu ya timu za taifa, klabu hizo zilikuwa zinahofia kuwa baada ya wachezaji kurejea wangetakiwa kukaa karantini kwa siku angalau 10.

Wachezaji wa Argentina Emiliano Martinez, Emiliano Buendia, Giovani Lo Celso na Cristian Romero walipoenda kwenye mechi ya kufuzu dhidi ya Brazil walipeleka mchezo huo kuahirishwa kutokana na kukiuka misingi ya Covid-19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live