Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AC Milan yaomba huruma kwa Matty Cash

 Methode Times Prod Web Bin 26e35bfa 60a4 11ee Aae8 B941e584b333 Matty Cash

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

AC Milan inaishawishi Aston Villa ikubali kupunguza bei ya beki wao wa kulia na Poland, Matty Cash, 26, ili ifanikishe mpango wa kumsajili katika dirisha hili la majira la kiangazi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Athletic, Villa inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni ili kumuuza Cash ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Beki huyo anayepanda na kufunga mabao yuko katika ubora wake. Milan imevutiwa na kiwango cha Cash kwa msimu huu alichoonyesha ndani ya England na kwenye michuano ya kimataifa.

WAKALA wa kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz, ameripotiwa kuwa katika mazungumzo na mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona, Deco ikiwa ni katika mipango ya staa huyo kujiunga na wababe hao wa Nou Camp katika dirisha hilo. Luiz mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akitajwa kwamba huenda akajiunga na Juventus ama Arsenal lakini kujitokeza kwa Barca kunaweza kusababisha upepo kubadilika.

CHELSEA inafikiria kuachana na mchakato wa kutaka kumuuza kiungo wake Conor Gallagher, katika dirisha hili badala yake inataka kumwongeza mkataba. Raia huyo wa England mwenye umri wa miaka 24, tangu mwezi uliopita tetesi zilidai kwamba huenda angeuzwa na timu iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kumsajili ni Tottenham.

Conor mwenye amekuwa akipinga suala la kuuzwa na mara kadhaa alizowahi kuhojiwa alisema anataka kubaki na kupambania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.

CHELSEA imeendelea kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuhakikisha inaipata saini ya straika wa Bournemouth, Dominic Solanke, 26, katika dirisha hili.

Solanke ambaye katika msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 21, aliwahi kuitumikia Liverpool. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

WOLVES inahitaji Pauni 45 milioni kutoka kwa timu yoyote itakayohitaji kumsajili beki wao kisiki, Max Kilman, 27, katika dirisha hili.

West Ham ni miongoni mwa timu zinazohusishwa kutaka kumsajili Kilman lakini inasua sua kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na Wolves. Mkataba wa Kilman unamalizika mwaka 2028.

WEST Ham imevutiwa na mshambuliaji wa Juventus, Matias Soule na inataka kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

Staa huyu wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 21, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliomalizika alicheza mechi 39 za michuano yote na kufunga mabao 11.

WEST Ham imeanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Udinese, Nehuen Perez, 23, katika dirisha hili baada ya kutuma wawakilishi wake kwenda Italia ili kufanikisha mchakato wa kumsajili.

Mkataba wa Nehuen unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kutoa asisti moja.

Chanzo: Mwanaspoti