Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AC Milan yakwea kileleni Serie A

Giroud Olivier Mshambuliaji wa AC Milan, Olivier Giroud

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

AC Milan wamevuna alama tatu za kibabe dhidi ya Napoli katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, na Arsenal Olivier Giroud.

Straika huyo wa Ufaransa French alikwamisha mpira nyavuni akimalizia pasi ya Davide Calabria kwenye ungwe ya kwanza.

Ushindi huo unaifanya Milan kufikisha pointi 60 alama mbili pungufu ya vinara Inter Milan ambao walishinda bao 5-0 dhidi ya Salernitana na alama tatu zaidi ya wapinzani wao Napoli.

Taarifa nyingine nzuri kwa kocha wa AC Milan Stefano Pioli ni kurejea kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live