Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AC Milan washika usukani Serie A

Ac Milan V Us Salernitana Serie A 3 AC Milan waibuka na ushindi Serie A

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha AC Milan kimeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Salernitana ushindi ambao umeifanya kukwea mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Seria A huku wakitoa heshima maalumu kwa mlinzi wao Simon Kjaer aliyepata majeruhi yatakayomfanya kuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima.

Kiungo mshambuliaji Franck Kessie aliitanguliza mapema kabisa AC Milan akipokea mpira mzuri kutoka kwa Rafael Leao kabla ya Alexis Saelemaekers kuongeza bao la pili kwa Milan, ambapo baada ya goli hilo alikimbia kuelekea kwenye bechi la timu yake na kushika jezi ya Kjaer ikiwa ni ishara ya pole.

Kjaer, itakumbukwa ndiye aliyekuwa mstari wa mbele katika kuokoa maisha ya Christian Eriksen katika michuano ya Euro 2020, alikutwa na majeruhi ya goti katika mchezo wa Ligi dhidi ya Genoa ambapo Milan ilishinda bao 3-0.

Matokeo hayo yanaifanya AC Milan kuwa juu ya Napoli ambao wanaweza kurejea kileleni endapo watashinda mchezo dhidi ya Atalanta utakaopigwa usiku wa leo Jumamosi Disemba 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live