Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

A-Z yaliyomkumba Aziz KI nchini Morocco

Aziz Ki Tena A-Z yaliyomkumba Aziz KI nchini Morocco

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amewatoa hofu mashabiki wa timu yake kuhusiana na hali yake baada ya tetemeko la ardhi lililotokea nchini Morocco huku akitumia nafasi hiyo kutoa salamu za pole kwa waathirika wa tukio hilo.

Aziz Ki yupo nchini Morocco ambako alienda na timu yake ya taifa ya Burkina Faso kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kufuzu ushiriki wa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Eswatini mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Stade de Marrakech, Marrakesh Morocco, ulioalizika kwa suluhu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aziz Ki alisema haikuwa hali ya kawaida, walihisi kishindo na kuanza kuulizana nini shida baada ya hapo kila mmoja alianza kujihami na kukimbia hadi walipokusanyika kwa pamoja.

“Haikuwa hali ya kawaida ulikuwa ni mshtuko mkubwa, benchi la ufundi lilifanya kazi kubwa kuhakikisha wanatukusanya pamoja ili kukwepa adha ya kuanza kutafutana moja moja na baada ya tukio hilo walitujenga kisaikolojia ili kutuondoa kwenye hali ya taharuki;

“Haikuwa rahisi kwani kila mmoja alikuwa anatafuta njia yake ya kujiweka kwenye usalama lakini viongozi wa timu yetu hawakuwa nyuma kutuweka pamoja ili tuweze kupata nafasi ya kuzungumza na kusahau kilichotokea.”

Alisema amepokea simu nyingi kutoka kwa viongozi, marafiki familia na ndugu wa karibu ambao walitaka kupata ufafanuzi kuhusiana na tukio lililotokea huko.

“Haikuwa rahisi kupokea simu kwa muda huo kwani mambo yalikuwa ni mengi lakini mara baada ya muda tuliruhusiwa kushika simu ili kuzungumza na familia kuwatoa kwenye hali ya huzuni;

“Natoa pole kwa familia zilizoathirika na tukio hilo na kuwaombea majeruhi Mungu awape afueni warudi kwenye hali zao za kawaida pia nawashukuru watu wote walionitafuta na kunijulia hali yangu, nipo salama mimi pamoja na wachezaji wenzangu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live