Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

A-Z Eng. Hersi alivyomsotea Chama mpaka kumnasa, mshahara wake kufuru

Chama Yanga 003 Clatous Chota Chama

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari Yanga wamekamilisha dili la Mwamba wa Luska, Clatous Chota Chama na kumtambulisha rasmi kama mchezaji wao mpya. Ni ishu ambayo ilikuwepo muda mrefu kwani Yanga walianza kumuinda Chama muda mrefu na mazungumzo yamechukua kipindi kirefu mpaka kukamilika kwake.

Chama ilikuwa asaini mkataba tangu Janurari mwaka huu wakati wa dirisha dogo la usajili. Kuna kipindi ambacho Chama alichelewa kujiunga na kambi ya Simba wakati Yanga wakikamilisha dili hilo lakini kuna mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii alitibua baada ya kupost picha ya Chama akiwa sehemu flani ikiashiria kabisa ni (Yanga).

Mwamba aliwahadaa viongozi wa Simba kuwa amepata dili Omani, baada ya hapo dili liliyeyuka kwani viongozi wa Simba walishtukia mchezo na kumnyima release letter ambayo ingemruhusu kuondoka. Hivyo alishindwa kuondoka kwa sababu hiyo.

Ndoto ya Chama imekuwa pale pale kwamba lazima ipo siku moja atacheza Yanga kwani ndiyo timu ya kwanza kumleta Tanzania mwaka 2027 lakini walishindwana akaelekea Simba.

Kwenye dili hili Chama tayari alikuwa ameshakubaliana na viongozi wa Yanga kuhusu mshahara, bonsai na maslahi mengine kwa muda mrefu ikizingatiwa kuwa alikuwa amebakisha mkataba wa miezi sita tu na Simba, hivyo ilikuwa inaruhusiwa kufanya makubaliano na klabu yoyote. Mwezi Aprili Yanga wakarudi tena kwa Yanga na akasaini mkataba.

KWA NINI CHAMA ALIIKUBALI YANGA Chama pale Simba alikuwa akilipwa dola 11,000 kwa mwezi nyuma ya Luis Miquissone aliyekuwa akilipwa dola 20,000 kwa mwezi, Simba wakampa Chama ofay a mshahara wa dola 9,000 wakiamini kuwa kiwango chake kimeshuka na umri wake umesogea, Simba hawakuamini kumuongezea mshahara bali kumpunguzia kwa sababu kiwango na umri imekuwa changamoto, Chama aligoma kusaini mkataba.

Chama hakuishia hapo, akaweza wazi kwamba anahitaji kuondoka ndani ya Klabu hiyo kwa sababu viongozi wa Simba wanamtuhumu kwamba anaihujumu timu na kuuza mechi, ni jambo ambalo lilikuwa likimkera sana Chama.

MSHAHARA WAKE Chama ni miongozi mwa wachezaji wachache matajiri sana Zambia na hapa Tanzania, pesa kwake sio tatizo bali anapenda kuwa na Amani sehemu anapofanya kazi, aheshimiwe na kuthaminiwa. Kutokana na tuhuma nyingi kumwandama, mwamba aliweka wazi kuwa anataka kusepa.

Chama amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga na anakwenda kulipwa mshahara wa dola 15,000 kwa mwezi ni nyuma ya Stephanie Aziz Ki ambaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Yanga. Pacome, Chama, Aziz Ki wote watacheza Yanga msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live