Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

5G za Yanga zatua Bungeni

Yanga Nzengeli Mzize.jpeg 5G za Yanga zatua Bungeni

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikao vya Bunge vinaendelea mjini Dodoma, lakini nje ya Bunge timu ya Yanga ya Dar es Salaam imefanya balaa lake kwa kugawa dozi ya 5G katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga iliifunga KMC mabao 5-0, pia ikaifunga JKT Tanzania idadi kama hiyo ya mabao katika mechi mbili ilizocheza za ligi hiyo msimu huu wa mwaka 2023/24, hivyo kuongoza ligi hiyo ikiwa na mabao 10 ya kufunga na haijaruhusu bao.

Unajua nini, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kumbe ishu nzima ya vipigo inavyotoa Yanga huko mtaani anayo bwana.

Iko hivi, leo Spika Tulia, baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu akawa anatoa taarifa kuhusu matokeo ya michezo mbalimbali katika bonanza la Bunge lililodhaminiwa na benki ya NMB Jumamosi mjini Dodoma.

Miongoni mwa matokeo aliyokuwa akisoma Spika Dk Tulia, kuna timu ilishinda mabao 3-0, alivyotaja hapo akasimama kidogo akasema kumbe ni mabao 3 nikajua mabao 5 kama anayofunga Yanga, hali ambayo iliibua shangwe kwa wabunge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live