Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

28 kunyukana RCL kuisaka First League

Malimao Pic Kikosi cha Malimao bingwa wa mkoa wa Katavi

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kumekucha. Ndivyo unaweza kusema baada ya shirikisho la soka nchini (TFF) kutangaza kuanza kwa ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) kwa timu 28 kupepetana katika hatua ya makundi, Machi 10 mwaka huu.

Timu hizo zimegawanywa makundi manne zikicheza katika vituo vya mikoa minne ikiwa ni Kagera, Kigoma, Shinyanga na Katavi ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Upande wa kundi A ni Buhaya (Kagera) ambao watakuwa wenyeji wakiwa pamoja na timu za Shilabela (Geita), Mapinduzi (Mwanza), Nyamongo (Mara), Damali (Simiyu), Nyumbu (Pwani) na Eagle ya Dar es Salaam.

Kundi B, Aglo Sports Academy itakuwa wenyeji mkoani Kigoma na Mambali ushirikiano (Tabora), Singida Cluster (Singida), Arusha City (Arusha), Tanesco (Kilimanjaro), Kiluvya (Dar es Salaam) na Kilosa ya Morogoro.

Maila Boys watakuwa wenyeji kwenye kituo cha Shinyanga ikicheza na Bus Stand (Dodoma), Aca Eagle (Manyara), Eagle Rangers (Tanga), Sharp Lion (Lindi), Mbuga (Mtwara) na Navy FC ya Dar es Salaam.

Malimao wao watakuwa nyumbani mkoani Katavi kwenye kundi D wakiwa na THB (Rukwa), Hollwood (Songwe) KFC (Mbeya), Ilula Tigers (Iringa), Zamalek (Njombe) na Mbinga United ya Ruvuma.

Afisa habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo amesema kila kituo kitatoa timu mbili za juu ambapo hatua ya mwisho itakuwa ni nane bora ambayo ni fainali.

“Ina maana kila kundi ni timu mbili na kutengeneza nane bora ambayo tunasema ni fainali na wale wawili vinara watapanda first league, tunazitakia timu zote maandalizi mema,” amesema Ndimbo.

Chanzo: Mwanaspoti