Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

22 kuiwakilisha Tanzania michezo ya wenye ulemavu wa akili duniani

10835143 6b0a 4fea Aec8 C6b7ff4177ea 22 kuiwakilisha Tanzania michezo ya wenye ulemavu wa akili duniani

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Mtanzania

Wachezaji 22 wenye ulemavu wa akili wanatarajia kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Dunia inayotarajia kuanza Mei 13 hadi Juni 12, 2023 Berlin Ujerumani.

Katika mashindano hayo Tanzania itawakilishwa na michezo miwili ambayo ni riadha na mpira wa wavu.

Washiriki hao walipatikana kupitia mashindano ya Taifa yaliyofanyika jijini Mwanza Desemba 2021 ambapo mchezo wa riadha ulifanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati wa soka na mpira wa wavu ilichezwa kwenye viwanja vya Sekondari ya Wavulana Bwiru.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mkurugenzi wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Charles Rays, amesema msafara huo pia utajumuisha makocha na wazazi wa watoto hao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, baadhi ya wachezaji watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Sheha Haji, Abdulrahman Shabani, Julius Francis, Uwesu Salim, Ally Nassor Juma, Duncan Anaclet, Emmanuel Chano na Mathias Makanyaga.

Wengine ni Fatuma Hashim, Maimuna Juma Ally, Judith Mbila na Nzobinimana Claudine.

Aidha amesema ili kufanikisha ushiriki wa mashindano hayo ya Dunia zinahitajika Sh milioni 195.

Mwaka 2019 mashindano hayo yalifanyila Abu Dhabi Dubai na kushirikisha nchi 183 ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu mbili za riadha na wavu. Mmoja wa wachezaji, Khalifani Ally Jihadi alishiriki mbio za mita 200 na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu.

Chanzo: Mtanzania