Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

18 waondoka Stand United

Stand United 18 waondoka Stand United

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Stand United ‘Chama la Wana’ imekiri kuondoka kwa nyota wake takribani 20 katika kipindi cha dirisha dogo kumewarudisha nyuma na kutibua mipango ya kupanda Ligi Kuu, wakieleza kuwa kwa sasa wanapambania pointi 32 ili kubaki Championship.

Timu hiyo iliyowahi kutesa Ligi Kuu na kuuteka mji wa Shinyanga ilishuka daraja misimu minne nyuma na sasa inashiriki championship ikiwa nafasi ya tisa kwa pointi 22.

Katika dirisha dogo ambalo limefungwa usiku wa kuamkia leo Jumanne Januari 16, timu hiyo imebomolewa kwa kuchukuliwa wachezaji 18 akiwamo kipa, Paul Kampele na beki wa kushoto, Berege Jamal waliouzwa Ken Gold.

Meneja wa timu hiyo, Fredy Masai amekiri kuwa kuondoka kwa nyota hao ni pengo kubwa, lakini kwa kutambua mpira ni maisha waliamua kuwaruhusu kuondoka kutafuta fursa.

Amesema kutokana na mabadiliko hayo wamejaribu kusuka upya kikosi huku akieleza kuwa hesabu zao za kupanda Ligi Kuu zimefifia na badala yake wanasaka pointi 32 ili kubaki Chmapionship.

“Lazima tukubaliane na mabadiliko kwa sababu mpira ni maisha, wengi waliomba kuondoka tukawaruhusu baada ya kupata fursa kwingine, tumeuza wawili pekee na tumesuka upya timu,” amesema Masai.

Meneja huyo ameongeza kuwa kwa sasa wanaendelea kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Pamba utakaopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Chanzo: Mwanaspoti