Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wingi wa talaka wamshtua Askofu Malasusa

33342 Pic+malasusa Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa  amesema ikilinganishwa na miaka ya nyuma hivi sasa Tanzania utoaji wa talaka umeongezeka.

Askofu Malasusa ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 25, 2018  katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Amesema wanandoa wengi wanaishi kwa hofu ya kutokuwa na hakika na maisha ya ndoa kutokana na kushamiri kwa talaka.

“Siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema.

“Malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanaume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu.”

Amesema ni vigumu kupaka rangi katika dhambi, hivyo kuiondoa ni njia rahisi zaidi, “Hatuwezi kupaka rangi kwenye dhambi, tunashuhudia masuala ya ushoga, ndoa za utotoni na mambo mengine mengi zikiwemo talaka.”

 



Chanzo: mwananchi.co.tz