Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Wenzetu wameuthaminisha muziki wa Injili kama miziki mingine" -Joel Lwaga

Joel Lwaga Mifupani Mwimbaji wa Gospel, Joel Lwaga

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Star wa muziki wa nyimbo za injili nchini, Joel Lwaga amesema kuwa moja ya vitu vinavyofanya muziki wa Injili usipige hatua kubwa hapa nchini ni kitendo cha kutofautisha muziki wa injili na miziki mingine jambo ambalo sio sahihi.

Lwaga amesema katika vitu ambavyo ameviona kutoka nchi tofauti tofauti alizotembelea na anatamani kama kingekuwepo hapa nyumbani ni kutokuwa na Utofauti kati ya muziki wa injili na muziki wa dunia

"Wenzetu wameshapata thamani ya muziki wao, nilienda Ghana kule hakuna tofauti kati ya muziki wa injili na muziki wa dunia, kwanza hakuna tuzo za gospel, tuzo ni moja tu wanashiriki wasanii wote, wa gospel na wasanii wa muziki wa dunia, kama ukitaka kuchukua tuzo basi shindana na wasanii wa muziki wa dunia"

"Tunajichelewesha sana kwenye hili, na hii huwa ninawachangamotisha mwanamuziki wenzangu wa gospel mara nyingi kwamba acheni kujifungia, mnajifungia sana, hii inatuchelewesha" amesema Lwaga

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha E-fm, kupitia kipindi cha "Empire" Lwaga amesema hata ujio wake tu katika kipindi kama hicho watu wanaona si sahihi jambo ambalo anapingana nalo kwa nguvu zote.

Lwaga amewataka wasanii wa muziki wa injili kutojiwekea mipaka kama kweli wanataka kuona maendeleo ya muziki wa injili hapa nchini.

Wanamuziki wa nyimbo za Injili akiwemo Goodluck Gozbert, wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa sana na vipingamizi pale ambapo wanajaribu kuingiza ama kuimba muziki wa injili kama nyimbo za muziki wa kizazi kipya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live