Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waumini wakumbushwa kuwapenda kina mama

53592 Pic+waumini

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Jamii imetakiwa kuwa na upendo kwa wanawake na kuishi maisha ya kuwa wakweli.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 22,2019 na askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Eusebius Nzigirwa wakati wa ibada ya shukrani ya Pasaka na utume wa uimbaji.

Katika mahubiri yake, Askofu Nzigirwa amesema wanawake ndio waliokuwa wa kwanza kutangaza furaha baada ya kupewa habari njema ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

“Katika maisha tujifunze kuwa na upendo na kina mama kwa kuwa ndio waliokuwa wa kwanza kutangaza habari njema za kufufuka kwa Yesu Kristo, ”amesema Askofu Nzigirwa na kuongeza kuwa katika maisha tunapaswa kutangaza ukweli kwa kuwa daima hauwezi kufunikwa na uongo.

“Tujitahidi katika maisha tunayoishi kuwa wakweli, ni rahisi mtu kuamini uongo kuliko ukweli lakini daima ukweli hauwezi kufunikwa na uongo,” alisema

Ameongeza, “Hkuna haja ya kuishi kimashaka, kwenye suala la kiimani tunapaswa kuwa wepesi kupokea ujumbe wa Mungu ili kukabiliana na magumu.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akitoa salamu za Pasaka, amesema waimbaji wanapaswa kufikisha ujumbe popote wanapokwenda.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz