Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 14 waliokuwa wasafiri na ndege iliyoanguka, wabadilishiwa usafiri

76963 Pic+ndege

Mon, 23 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Wageni 14 waliokuwa wanakwenda kuchukuliwa na ndege iliyopata ajali uwanja wa Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania na kusababisha vifo vya watu wawili akiwamo rubani wamepewa usafiri mwingine.

Ndege hiyo ya kampuni ya Auric air yenye namba 5H-AAM iliyokuwa inaendeshwa na Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania, Venance Mabeyo imepata imeanguka leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019.

Katika ndege hiyo kulikuwa na Nelson na Nelson Orutu ambaye inadaiwa ni rubani mwanafunzi lakini si wa kampuni hiyo ambo wote kwa pamoja walifariki ndani ya ndege hiyo iliyoanguka muda mfupi baada ya kuruka kwenda kuwabeba wageni hao waliokuwa Grumeti Kirawira.

SOMA ZAIDI:  Mtoto wa mkuu wa majeshi Tanzania afariki ajali ya ndege

Msimamizi wa kampuni hiyo kwa Serengeti,  Peter Kimaro ameiambia Mwananchi kuwa wamebadilisha safari za ndege zao mbili na kwenda kuwachukua wote na kuwapeleka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

"Wageni hao walikuwa wa kampuni ya And beyond Tanzania na sisi tulikodiwa kuwasafirisha, baada ya tukio tukachukua hatua ya haraka maana wale walikuwa na ratiba yao," amesema.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
SOMA ZAIDI

>Helikopta ya JWTZ yatua Serengeti kuchukua mwili wa mtoto wa Mabeyo

Chanzo: mwananchi.co.tz