Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa familia moja wafa maji wakiogelea

20312 Watoto+Pic TanzaniaWeb

Tue, 2 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kijiji cha Tabaruka wilayani Sengerema wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye kisima kilichopo kijijini hapo.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba Mosi, 2018 mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amewataja watoto hao kuwa ni Given Aloyce (14) na Tekla Aloyce (12) waliokuwa wakisoma shule ya Msingi Tabaruka.

Kipole amesema tukio hilo limetokea Septemba 29, 2018  saa 11:00 jioni kijijini hapo walipokwenda kwenye kisima kufua sare za shule.

“Hawa watoto walikuwa na mwenzao Japhet  Daud, lakini yeye hakuogelea alikuwa akiwatazama,” amesema Kipole.

Daudi ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema baada ya kuona wenzake wanazidiwa na maji alikimbia nyumbani kwao na kutoa taarifa ili apate msaada wa kuwaokoa.

Mjomba wa watoto hao, Renatus Zakaria amesema ndiye alifika eneo la tukio akiwa wa kwanza na kuopoa miili ya watoto hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema hajapata taarifa hizo lakini anafuatilia.

Baba wa watoto hao, Aloyce Kashirimu amesema baada ya kupata taarifa hizo alikimbia hadi eneo la tukio lakini alikuta tayari miili yao imeshaopolewa na wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz