Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watakiwa kutenga muda kumtafuta Mungu

34335 Pic+ushauri Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watanzania wametakiwa kutenga muda wao kumtafuta Mungu baada ya mihangaiko ya siku kwa siku kushughulikia maisha yao.

Hayo yamesemwa leo Januari Mosi, 2019 na msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mchungaji Chediel Lwiza, wakati akiongoza ibada ya mwaka mpya 2019 katika kanisa la KKKT Azania Front.

Amesema kuhangaikia maisha pasipo kumtafuta Mungu hakuna baraka na ni maisha yasiyo na maana.

Mchungaji Lwiza amesema ikiwa maua ya kondeni, ndege wa angani hawalimi wala hawavuni lakini Mungu anawapa malisho yao, haina maana kwa mwanadamu anayehangaikia maisha akimsahau muumba wake.

“Kufanya kazi kwenu siku kwa siku mahangaiko hayo yanaweza yakachukua nafasi ya Mungu. Katika kufanya kazi, kushughulika kunakoondoa nafasi ya Mungu ni kitu kibaya kwa maisha ya mwanadamu,” amesema Mchungaji Lwiza.

Katika ibada hiyo, mamia ya waumini wanajumuika pamoja katika misa ya kwanza ya siku ya kwanza ya mwaka, huku wakitakiana heri na mafanikio katika mwaka mpya 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz