Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watakiwa kusahau machungu ya 2018

34329 Pic+watanzania Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ngara. Watanzania wametakiwa kusahau magumu yaliyowatesa mwaka 2018 na kumuomba Mungu kuwabeba katika matukio yenye kuwaletea amani na utulivu ndani ya mipango ya kujiletea maendeleo kwa mwaka 2019.  

Wito huo ulitolewa jana Desemba 31, 2018 na Askofu wa Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Kagera, Darlington Bendankeha wakati wa ibada ya kuuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2019 iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Murugwanza mjini Ngara.

Askofu Bendankeha alisema mwaka 2018 kuna matukio ya kusononesha na kuumiza jamii yaliyotokea ambayo yanatakiwa kuombewa yasijirudie mwaka mpya wa 2019.

“Waumini wa madhehebu ya dini nchini hatuna budi kujenga utamaduni wa kusameheana katika yote na kujenga Taifa bora sasa na baadaye,” alisema Askofu Bendankeha

Alitaja kupungua kwa upendo, kuenea kwa hasira na chuki miongoni mwa wana jamii kuwa ni kati ya mambo yaliyojitokeza mwaka uliopita yanayostahili kuachwa kwa kila Mtanzania kutanguliza upendo, mshikamano na undugu kwa wote.

Alisema wananchi wa kawaida, wanasiasa na viongozi wa Serikali na madhehebu ya dini wana wajibu si tu wa kuhimiza upendo, bali kuujenga kwa kutenda haki kwa wote, kuheshimiana, kujadiliana na kusikilizana.

Akizungumza wakati wa ibada hiyo, Mchungaji Kanoni Fares Sendegeya aliwasihi viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kutimiza wajibu na majukumu kwa njia ya haki kwa kila mtu na makundi ya kijamii.



Chanzo: mwananchi.co.tz