Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wahamasishwa kusaidia wahitaji

C17d72c5dd0e100c2b384abc2c0e387e Taasisi zaki Dini

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI za Kidini nchini zimetakiwa kuhamasisha umoja na amani kwa Watanzania pamoja na kusaidia jamii kupitia huduma mbalimbali kama vile elimu na afya.

Akizungumza wakati wa matembezi ya amani Dar es Salaam, Katibu wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna’Asheri, Imran Sherali, amesema Tanzania itaendelea kuwa nchi salama endapo watahamasishana upendo, mshikamano na kutobagua rangi wala dini.

"Leo hii dunia inahitaji amani na upendo mani na lengo la kuwa na matembezi haya kwa ajili ya Imam Hussain (as) ni kutaka kupaza sauti kwamba amani, utulivu na upendo ni moja ya jambo muhimu na lienziwe na liangaliwe kwa makini," amesema Sherali.

Amesema alikuwa ni mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuliwa kikatili na mwili wake kukatwa katika jangwa la Karbala akiwa anatetea dhuluma kwa binadamu, hivyo ili kumuhenzi Ashura ni pamoja na kusaidia jamii kwa kujitolea damu na kutoa huduma nyingine za afya.

Amesema Watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwa na upendo kwa kila mtu kwa kujitolea kusaidia mambo ya jamii ikiwemo kuchangia damu.

Amesema jumuiya hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ikiwemo kutoa huduma bora za afya kwa gharama nafuu kupitia hospitali zao za Ebrahim Haji.

Pia alisisitiza kubwa wameanzisha kituo cha matibabu ya macho na mtoto wa jicho kwa gharama nafuu ili watanzania wenye uhitaji kupata huduma hizo kwa urahisi.

Pia amesema wanashirikana na Kituo cha damu salama kuhakikisha kila mwaka wanachangia damu ili kuokoa maisha ya mama wajawazito na watu wenye uhitaji wa damu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz