Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania kutokwenda Hijja Makka

Cef806ed022eb73a839a49c68226dfd3 Watanzania kutokwenda Hijja Makka

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BAZARA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limesema mwaka huu hakutakuwa na lbada ya Hijja kwa mahujaji wa Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine zote duniani kutokana na zuio lililowekwa na Serikali ya Saudi Arabia.

Zuio hilo linatokana na kusambaa kwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 unaoisumbua dunia.

Mufti wa Tanzania na Shehe Mkuu, Abubakar Zubeir alisema jana kuwa taarifa alizopewa na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini, Abdulaziz Hamad ni kwamba Hijja itatekelezwa na wananchi wa Saudi Arabia na wageni ambao ni raia wa taifa hilo peke yao.

Alisema Serikali ya Saudi Arabia kupitia wizara yake ya Hijja wameona kwamba mwaka huu waifute Hijja kwa nchi zote za nje ibakie Hijja kwa wananchi wa nchi hiyo peke yao kwa idadi ndogo ya mahujaji 60,000.

“Kwa hiyo nawaarifu Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa masuala ya Hijja mwaka huu hakuna, badala yake wajiandae kwa Hijja mwaka ujao na Mwenyezi Mungu atupe subira juu ya jambo hili na atuvishe uchamungu kwa sababu huu ni mwaka wa pili hatuendi Hijja,” alisema Mufti.

Kuhusu watu ambao tayari walishajiandikisha na kulipia safari ya Hijja, Shehe Zubeir alisema utaratibu wa kwenda Hijja unaratibiwa na kusimamiwa na Taaisi ya Tanzania Hajj Mission inayojiendesha chini ya uratibu na usimamizi wa Bakwata.

Alisema kutakuwa na utaratibu maalumu ambao utatangazwa na taasisi ya Tanzania Hajj Mission juu ya namna gani kwa wale waliotoa fedha zao ama watarudishiwa au kuzibakiza katika akaunti ili zitumike katika Hijja ya mwaka ujao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz