Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania endeleeni kutunza amani- Mhubiri

586e816097a93880e8719f6ab5c4267b.png Watanzania endeleeni kutunza amani- Mhubiri

Sat, 14 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MHUBIRI wa kutoka Marekani, Mwinjilisti Dk Dana Morey amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani waliyonayo, waendelee kuwa mfano kwa mataifa mengine.

"Watanzania muendelee kumshirikisha Mungu zaidi kwani nchi nyingi wanaitamani amani yenu, Mungu amewaletea amani ambayo nchi nyingine wanaitamani, hivyo ninawaomba mtunze ili iwe mfano hata kwa mataifa mengine ambayo hawana amani na utulivu," alisema.

Alisema hayo juzi wakati akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu, unaofanyika jijini hapa ambao umeambatana na semina ya neno la Mungu.

Aliwataka Watanzania kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, wanalolifanya ili waweze kubarikiwa zaidi na kuishi kwa amani na utulifu, huku wakitangaza habari njema za utukufu.

Akizungumza katika mkutano huo wa injili, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge aliwahamasisha viongozi wa madhehebu ya dini, kuchangamkia fursa ya viwanja vinavyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili wawekeze kwenye huduma mbalimbali ikiwemo ya kiroho na kijamii.

"Watumishi wa Mungu mnatakiwa kuchangamkia muweze kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na kiroho," alisema.

Alishukuru viongozi wa madhehebu ya dini, kuhamasisha waumini wao kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu na kuweza kufanyika kwa uhuru na usalama.

Chanzo: habarileo.co.tz