Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waomba ushirikiano kupinga ukatili wa kijinsia

9a4424780e42607aeea527bf65949ee0 Waomba ushirikiano kupinga ukatili wa kijinsia

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa dini na wadau mbalimbali nchini wameshauriwa kushirikiana kukabili vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo ambalo litasaidia familia na nchi kuwa na amani.

Aidha wanaume wamehimizwa kujitokeza na kupaza sauti kuhusu matukio ya vitendo vya ukatili kwa kuwa vimekuwa vikifanyika lakini wakikaa kimya bila kutoa taarifa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa kitaifa wa Taasisi ya Walking the Giant Initiative, inayofanya kazi kupitia Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Mchungaji Modest Pesha alisema ipo haja ya kufanya mazoezi ya mwili kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Alisema katika makanisa mbalimbali yapo madawati ya utetezi wa kijinsia yanayotetea haki za wanaume, lakini pia katika Dayosisi kuna idara za malezi hivyo Kanisa na hata wadau wengine waendelee na mchakato wa kutoa elimu kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili.

“Ni muhumu sasa kwa viongozi wa dini kutumia madarasa mbalimbali ya watoto ili wapewe elimu kama madrasa na hata mafundisho ya kipaimara ili watoto nao waweze kuelewa na kupaza sauti wanapoona vitendo hivyo," alisema Mchungaji Pesha.

Alisema viongozi wa dini na wadau wanapiga kelele na wengine, kuelimisha jamii kwa ajili ya kupaza sauti kupinga vitendo vya kikatili nchini ili kuwa na jamii iliyostaarabika.

“Vitendo vinaendelea kufanyika na elimu zaidi inahitajika, mafundisho ya kiimani pia yanaweza kusaidia kupunguza vitendo hivyo, bado wapo ambao wanahitaji mabadiliko,” alisema.

Kuhusu mazoezi ya viungo vya mwili alisema ni ya muhimu zaidi kiafya, kiimani kama ilivyo kufunga na kuomba hivyo kuwe na mchakato endelevu, utakaosaidia kutunza saikolojia na kulinda afya ili kuwepo na ugumu kwa mtu kumtendea mwingineukatili kwa kuwa atakuwa safi kiakili.

Alisema kila mtu atimize wajibu wake na ukatili utakimbia na kuwataka wanaume wanaopata ukatili wa kijinsia kujitokeza ili kujua hali ikoje.

Mkurugenzi wa wanawake na watoto katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K KKT ) Faustina Losai ambaye pia anasimamia masuala ya haki na usawa wa kijinsia katika kanisa na jamii alisema Kanisa hilo lina mpango wa kuhakikisha haki na usawa jinsia katika kuondoa tofauti zote kwa kushirikiana na watu wa imani mbalimbali kwa kuwa ukatili unamgusa kilammoja.

Alisema taasisi mbalimbali za kiimani na kijamii zinaungana pamoja kupaza sauti kutokomeza ukatili ambao umekuwa ukiwakumba wanawake na watoto na Tanzania iko mstari wa mbele kutokomeza hilo.

Mwenyekiti Taifa wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania chini ya Bakwata, Hajat shamim Khan alisema vitabu vya dini vimekataa ukatili na kusisitiza kuwa wanawake na wanaume ni sawa.

Alisema hakuna vitabu vya dini vilivyohalalisha ukatili na kuwataka wanawake kuzijua sheria mbalimbali ili zile ambazo bado zinaendeleza ukatili ziweze kuondolewa lengo kubwa likiwa ni kutokomeza vitendo hivyo nchini.

Chanzo: habarileo.co.tz