Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaokula hadharani mchana wakati wa Ramadhani kukamatwa

Chakula Mwehhh Wanaokula hadharani mchana wakati wa Ramadhani kukamatwa

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka Kaskazini mwa taifa la Nigeria Polisi wa Kiislamu wametumwa Misikitini ili kuhakikisha usalama wa maisha na mali za Wananchi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya jana Alhamisi, Jeshi la polisi la kidini linalojulikana kama Hisbah Board, lilionya kwamba wale wanaojihusisha na maovu ya kijamii katika mwezi huu mtakatifu wataadhibiwa.

Kamanda mkuu wa bodi hiyo Harun Ibn-Sina, alinukuliwa akisema kuwa baadhi ya vijana wanaokula hadharani wakati wa mfungo pia hawatasalimika.

Bw Ibn-Sina alitoa wito kwa Waislamu kuwasaidia mayatima na wahitaji katika kipindi cha mfungo kilichoanza Alhamisi. Bodi ya Hisbah inatekeleza sheria hizi za Kiislamu huko Kano, jimbo ambalo lina Waislamu wengi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live