Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa watua mahakamani kudai haki ya kumpatia mtoto wao jina la kuzimu

Nyie Mtoto Wanandoa watua mahakamani kudai haki ya kumpatia mtoto wao jina la kuzimu

Sat, 25 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanandoa hao Kristina Desgres na Rodrigo Velasquez walipata mtoto wao wa kiume mnamo Septemba mwaka jana.

Hata hivyo, hawana cheti rasmi cha kuzaliwa cha mtoto wao au ‘livret de Famille, kwa sababu mwendesha mashtaka wa umma wa Saint-Malo anakataa kuidhinisha jina la mtoto wa kiume, kama ilivyoripotiwa na Oddity Central.

“Hades” (Kuzimu)inajulikana katika hadithi za Kigiriki kama mungu wa ulimwengu wa chini, na wanandoa hao walisema jina hilo halikumshtua mtu yeyote baada ya mtoto wao kuzaliwa na walimchagulia jina hilo mtoto wao.

“Hakuna mtu alieshangaa baada mimi kujifungua nakumpa jina mwanangu, haikushtua mtu yeyote Kinyume chake, watu wamependa tulichagua  jina hili kwa sababu tu tulifikiri lilikuwa zuri yaani aitwe Hades Velasquez Desgres inasikika vizuri,” mama wa mtoto alisema

Hata hivyo, mwendesha mashtaka wa umma aliona jina la mvulana huyo halifai.

Aliongeza kuwa jina hilo halina madhara kwa mtu yeyote na alitaka uhalisi linapokuja suala la jina la mtoto wao: “Hatuelewi uamuzi huu.

“Hatuamini kwamba tumechagua jina la kwanza ambalo lina chuki kwake hatukumwita  Lusifa au Shetani, sisi si wajinga tulitaka tu jina la kwanza la asili, ambalo linasikika vizuri. Rodrigo baba wa mtoto alipopendekeza ‘Hades’ (kuzimu)kwangu, niliipenda mara moja.”

Mwanasheria aliajiriwa ili kusaidia kesi ya wanandoa kama walifanya utafiti zaidi na kujua kwamba wanandoa wengine wametoa jina moja kwa watoto wao bila shida  yoyote na zaidi ya hayo, waliwasiliana na wazazi ili kuona ikiwa watoto wao walikua bila masuala yoyote ya kuchezewa/utani kwa jina kama hilo.

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wake Aprili 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live