Unguja. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Fuoni Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar wameukata uongozi wa shule hiyo kuwadhibiti wenzao wanaokwenda shule wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na kuzificha chooni.
Wametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 23, 2019 katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wakawake (Tamwa) Zanzibar na dawati la jinsia la Jeshi la Polisi.
Mmoja wa wanafunzi , Abdalla Majid amesema mara kadhaa amewashuhudia wenzake wakivuta bangi chooni na nyingine kuzificha, kwamba hali hiyo inasababisha baadhi yao kuishia chooni badala ya kwenda darasani.
Summaya Kheri amesema baadhi yao huwa na nguo katika mabegi jambo linaloashiria kuwa huvua sare za shule na kuvaa nguo hizo.
Kuhusu udhalilishaji kwa wanafunzi, Saida Kheri ameuomba uongozi wa shule hiyo kujenga uzio, kwamba kukosekana kwake ndio chanzo cha kuibuka kwa udhalilishaji.
Akijibu kuhusu uzio, sheha wa shehia ya Fuoni Uwandani, Juma Mussa Juma amesema jitihada mbalimbali zimeanza kufanywa kujenga uzio huo.
Pia Soma
- Serikali ya Tanzania yawatema wahandisi 67 wa maji
- Adakwa na polisi kwa kujifanya polisi, daktari
- Iran yadai kukamata majasusi wa Marekani