Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakristo wahimizwa malezi mema kwa watoto

02fb6b6fc97b20ac68be94cded1a0ffc.png Wakristo wahimizwa malezi mema kwa watoto

Wed, 7 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKRISTO wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili ya kumpendeza Mungu ili wakue katika misingi ya kulipenda taifa na kuwa wazalendo wa nchi yao.

Wito huo ulitolewa juzi na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa Kuu Dodoma, Evance Mwaonga wakati wa ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyoambatana na ubatizo wa watoto zaidi ya 40.

Alisema wazazi wanatakiwa kuwafundisha na kuwapa malezi mazuri watoto wao tangu wakiwa wadogo ili taifa liweze kuja kuwa na vingozi waadilifu na wacha Mungu.

"Watoto wasipolelewa katika misingi iliyobora taifa haliwezi kuwa na vijana wawajibika, haliwezi kupata viongozi wenye hofu ya Mungu. Watoto hawa tuliowabatiza tuwafundishe mema kwa ajili ya kanisa na nchi yetu kwa ujumla."

“Vijana mkiona wazazi wenu tunaendi katika njia ambazo hazimpendezi Mungu mna jukumu la kuwakumbusha maandiko ya Biblia yanavyosema na wazazi pia mfanye vivyo vivyo kwa vijana wetu, hapo tutakuwa tunatekeleza vyema maneno ya Yesu chunga kondoo zangu," alisema Mchungaji Mwaonga.

Chanzo: www.habarileo.co.tz