Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakristo 100 kanisa moja wafungwa China

32004 China+pic TanzaniaWeb

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Beijing, China. Mchungaji maarufu wa China na mwanazuoni wa sheria ni mmoja wa Wakristo 100 waliofungwa na mamlaka baada ya kuripotiwa walikamatwa kwa madai ya "kuhamasisha uchochezi dhidi ya mamlaka ya Serikali." Wang Yi na mkewe, Jiang Rong, walichukuliwa na kuwekwa katika mahabusu ya polisi katika jiji la Chengdu wiki iliyopita, ambako wanaongoza Kanisa la Makimbilio ya Mvua Mapema, kwa mujibu wa ChinaAid, asasi ya Marekani inayofanya utetezi kwa niaba ya jumuiya za Wakristo wa China. Mfanyakazi katika kanisa hilo, ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake aliithibitishia CNN kwa njia ya simu juu ya kukamatwa kwa Wang. Maofisa wa Mamlaka ya Taifa kuhusu dini hawakujibu maswali waliyoulizwa na CNN. Serikali za nchi za Magharibi na watetezi wa haki za kiraia waishio nje ya China wamelaani kukamatwa kwa waumini wa parokia ya Kimbilio la Mvua ya Mapema kuwa ni hatua ya hivi karibuni ya Serikali ya China kukandamiza uhuru wa kidini. Vilevile, China imeshutumiwa hivi karibuni kwa kuendesha kampeni maalumu inayokiuka haki za binadamu dhidi ya mamia ya maelfu ya Waislamu wa Uyghurs katika mkoa wa Magharibi wa Xinjiang. China inasema hatua zake zinalenga kupambana na vurugu za wenye msimamo mkali na mara kwa mara imekuwa ikikanusha madai kwamba eneo hilo limegeuka kuwa la ukandamizaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz