Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu wahimizwa kulinda amani, mshikamano

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imewataka waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini kudumisha amani.

Pia viongozi wa dini ya kiislamu wamesisitiza umoja na mshikamano kwa waislamu na watanzania nchini.

Akizungumza leo Agosti 22 katika baraza la Edi el Hajj lililofanyika kitaifa viwanja vya Sikati Tamaa, Vingunguti, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, amewataka watanzania kwa ujumla kutafakari na kujifunza umuhimu wa kulinda amani.

“Ni muhimu kuangalia na kujifunza wka nchi zilizo katika machafuko, mnaona jinsi wanawake, watoto na wazee wanavyoathirika katika nchi zenye vita,” amesema.

Swala hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya kuchinja kwa waislamu wote duniani.  

Ibada hiyo iliyotanguliwa na hotuba ya viongozi wa dini, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiislamu na kisiasa akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

 “Sehemu ya Ujumbe wenu wa leo mliosoma hapa ni kudumisha amani, ujumbe huo serikali ingependa kuona unafika kila msikiti, madrasa, kila nyumba ya mwislamu na kiujumla kila nyumba ya mtanzania, amani ndiyo msingi wa kila kitu, maendeleo hayawezi kupatikana bila amani, mambo yote mazuri lazima amani iwepo kwanza,”amesema Dk Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi.

Awali, katika hotuba yake, Dk Mwinyi amefikisha salamu za Rais John Magufuli mbele ya baraza hilo, aliyeomba waislamu wote nchini kuendelea kumuombea katika uongozi wake huku akiwaomba kudumisha amani ya Taifa. 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz