Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu wahimizwa kuendeleza mema baada ya Ramadhani

6f9c1ac327029af761ba740a80ced955 Waislamu wahimizwa kuendeleza mema baada ya Ramadhani

Mon, 3 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAUMINI wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutenda mema hata baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Kauli hiyo ilitotelewa na Imamu wa Msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es Salaam, Shehe Issa Othman, wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered kwa ajili ya wateja na wafanyakazi na wateja wake juzi

"Mwezi wa Ramadhani ni wa toba, lakini haimaanishi kuwa miezi mingine tusifanye toba, hapana, tunatakiwa kujiweka katika matendo bora kila wakati kama ilivyoamriwa katika vitabu vitakatifu,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughan, alisema benki hiyo imeandaa futari hiyo kama ishara ya kurudisha fadhila kwa jamii kwani wanaposhukuru wanapata faida.

"Wanapofunga wanaomba na kutuombea hata sisi hivyo tunabarikiwa wote," alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz