Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu Tanzania waaswa kutunza amani, kuwasaidia wenye uhitaji

Wed, 14 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mirerani. Waislamu Tanzania Watanzania washauriwa kuwajali wahitaji na kutunza amani iliyopo kwani bila utulivu hakuwezi kufanyika maendeleo yoyote ya kijamii na kimaisha kwa ujumla.

Imamu wa Msikiti Noor Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara nchini Tanzania, Ustaadh Ramia Isanga ameyasema hayo kwenye swala ya Eid-El-Adh’aa, wakati akitoa ujumbe kwa waumini wa eneo hilo.

Ustaadh Ramia amesema mtu anapaswa kutunza amani aliyonayo, ya jamii inayomzunguka na ya Watanzania kwa ujumla ili kuendeleza maendeleo yaliyopo.

"Unapaswa kulinda amani uliyonayo binafsi, amani ya mwenzako na amani ya Watanzania wengine kwa lengo la kuhakikisha tunaenzi na kuitunza iliyopo kwani bila ya haki na amani hatuwezi kufanya chochote," amesema.

Amesema wakati huu wa sikukuu ya Eid-El-Adh’aa inapaswa wale wenye uwezo wawasaidie wasio na uwezo ili nao washerehekee sikukuu hii wakiwa na mioyo mikunjufu.

"Wale waliochinja wanapaswa kuwapa kitoweo wasio na uwezo na pia wawagawie mchele na fedha ili nao wafurahie sikukuu hii na kujisikia amani ya kutosha mioyoni mwao,” amesema

Pia Soma

Pia, amewataka Waislam kusherehekea bila kujihusisha na ulevi kwani siyo jambo zuri kunywa pombe na kulewa kwenye sikukuu kama hiyo.

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Haji Msham Ngokwe amesema sikukuu hiyo ya Eid-El-Adh’aa imekuja vizuri kwani jamii imesherehekea kwa amani kwa waumini wa dini ya kiislamu kwenda miskitini na kurudi nyumbani.

"Wito wangu ni wazazi kuwatunza watoto wao kwenye sherehe kama hizi kwani wanapaswa kufurahia kwa kiasi na siyo kugeuka kuwa karaha au matatizo ambayo yanaepukika," amesema Ngokwe.

Chanzo: mwananchi.co.tz