Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislam Tanzania watakiwa kudumisha amani

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waislamu wametakiwa kudumisha amani ya Tanzania kwa kutenda wema bila kujali itikadi na makundi ya watu ili Mungu aweze kuachilia baraka zaidi katika maisha yao.

Kauli hiyo imetolewa leo asubuhi Jumanne Juni 4, 2019 kwenye hotuba ya Eid el-Fitr ikiwa ni maadhimisho ya kuhitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu wa madhehebu ya Hansar Sunni.

“Ujumbe wa leo Waislam wahakikishe wanadumisha amani, kwa kuendeleza huruma na upendo kwa watu,” amesema Sheikh wa Msikiti wa Mabibo Relini, Haruna Kapama aliyeongoza swala katika viwanja vya Mabibo External jijini Dar es Salaam

“Al?amdulill?h Uislamu unaendana na matendo ya huruma kama tunavyoona kwa mnyama basi kwa binaadam ni zaidi. Wala hautazami binadamu huyu anayo itikadi ya aina gani.”

“Pia tunasisitiza wayaishi mafunzo wanayoyapata ndani ya Uislamu ili waendelee kuwa wema kwa sababu Dunia inahitaji watu wema, watu wanapokuwa wema basi Mungu anabariki katika maisha yao.”

Katika hotuba hiyo, Sheikh Kapama amewataka Waislamu wote kutii na kuwasikiliza viongozi huku akishauri viongozi pia kuwa na mapenzi, uadilifu na kujiepusha na dhuluma kwa raia.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz