Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanya Misa kumuombea Dk Magufuli

01d51904ca859bb4aa3372b15cbede90 Wafanya Misa kumuombea Dk Magufuli

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Benedeta ya Nzega Mjini wamefanya Misa Takatifu kwa ajili ya kumuombea pumziko la amani Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Dk Magufuli alifariki dunia Machi 17, mwaka huu, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya umeme wa moyo.

Akiongoza misa hiyo ofisi ya CCM wilaya ya Nzega, Paroko wa Parokia hiyo Padri Felix Kiko alisema kanisa linamuombea apumzike kwa amani baada ya kuutumikia umma wa Watanzania kwa weledi na uadilifu.

Dk Magufuli alizikwa Machi 26 mwaka huu wilaya ya Chato mkoani Geita

Alisema kanisa Katoliki limeguswa na msiba huo wa kuondokewa na kiongozi wa nchi ambaye aliipenda nchi yake na aliuchukia umaskini na kuendelea kuukuza uchumi wa nchi.

Padri huyo aliongeza kwa kusema kwa kushirikiana na CCM kanisa hilo limeifanya misa hiyo takatifu kwa ajili ya kumwombea hayati huyo ili apokelewe kwa amani.

Aidha, Paroko huyo aliwataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Sita , Samia Suluhu Hassan na kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na Hayati Magufuli.

Nao, viongozi wa CCM wilaya ya Nzega, akiwemo Katibu wa CCM wilaya Said Goha alisema wameiandaa misa hiyo kumuombea mpendwa wao Dk Magufuli.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega, Amosi Kanuda aliwashukuru wana CCM, wananchi na viongozi mbalimbali kwa kuhudhuria misa hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz