Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachungaji kupewa mbinu za kujikwamua kiuchumi

68842 Wachumgaji+pic

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wachungaji, manabii na mitume zaidi ya 500 wanatarajiwa kupewa mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi na kujitegemea ili kwenda sawa na lengo la serikali la kuwa na uchumi wa viwanda.

Mafunzo hayo ya siku tatu yatakayotolewa na kanisa la Agape yatafanyika kuanzia  Agosti 1 hadi 3 katika kituo cha Agape kilichopo  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi kiongozi wa kanisa hilo , Mtume Dk Vernon Fernandes alisema mafunzo hayo yanalenga kuwakomboa kiuchumi watumishi wa Mungu na kuwafanya kuwa sehemu ya watanzania wanaoshiriki katika kujenga uchumi wa kati.

Alisema, “Tunataka dhana ya umaskini na utegemezi iondoke, watumishi wengi wamejikita kwenye kuhubiri injili pekee na kusahau mambo mengine ya kijamii sasa hili linatakiwa kubadilika,”

Yale mawazo ya kutegemea misaada kutoka nje yanatakiwa kuondoka sasa, wenyewe tufikirie tunafanya miradi gani ili kukuza makanisa yetu huku tukilenga kuleta tija kwenye jamii. Unaweza kupanua kanisa na kufanya shughuli mbalimbali bila kutegemea misaada kutoka nje,”

Akitolea mfano wa kituo chake cha televisheni, shule na makanisa yake ,Dk Fernandes alisema alianzisha vyote hivyo bila msaada wowote kutoka nje ya nchi.

Pia Soma

“Tukiwa na miradi kwa namna moja au nyingine watumishi wa Mungu pia tutakuwa tunamuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kuifanya Tanzania ya viwanda. Tunaambiwa Yesu alilisha watu 5000 hii tunaweza kuitafsiri kama kiwanda maana kwa sasa kufanikisha hilo lazima uwe na kiwanda,”

Mafunzo hayo yatawakutanisha pia viongozi wakubwa wa dini akiwepo kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima, Askofu Zakaria Kakobe na Askofu Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International Sylvester Gamanywa.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz