Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge walijaribu kulazimisha kanisa kuzungumzia ndoa za jinsia moja-askofu

Wabunge Walijaribu Kulazimisha Kanisa Kuzungumzia Ndoa Za Jinsia Moja Askofu Wabunge walijaribu kulazimisha kanisa kuzungumzia ndoa za jinsia moja-askofu

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Askofu Mkuu wa Kianglikana, Mchungaji Justin Welby amesema "alitishiwa na hatua za bunge" katika jaribio la "kulazimisha ndoa za jinsia moja" katika Kanisa la Uingereza.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa Baraza la Ushauri la kanisa la Anglikana nchini Ghana.

Matamshi yake yanajiri baada ya mageuzi ndani ya kanisa kuruhusu wapenzi wa jinsia moja katika ndoa za kiraia.

Mabadiliko hayo yalifanywa baada ya hoja iliyopitishwa na Sinodi Kuu, chombo cha kutunga sheria cha kanisa hilo mwezi huu.

Msimamo wake kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja hautabadilika na wapenzi wa jinsia moja bado hawataweza kufunga ndoa kanisani.

Gazeti la Telegraph liliripoti kuwa Bw Welby alikutana na wabunge katika House of Commons mwezi uliopita, na waliotaka kufanyika kwa mabadiliko zaidi kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja.

Akizungumza kabla ya mabadiliko hayo, mtangazaji Sandi Toksvig alisema mkutano wa Januari na askofu mkuu, mwezi uliopita "ulikuwa wa kukatisha tamaa sana".

Bi Toksvig ni mwanaharakati mashuhuri wa masuala ya LGBT+, na ingawa sio mshiriki wa kanisa, aliambia BBC kuwa alizungumza kwa sababu alihisi athari ya ujumbe uliotumwa na maaskofu ulikuwa na athari za ziada katika Kanisa. .

Mabadiliko katika kanisa yamekuwa yasiyopendeza kwa baadhi ya wahafidhina, lakini pia yanapungukiwa na kile wapenda maendeleo wengi walikuwa wakitaka.

Akitoa hotuba ya rais Jumapili, Bw Welby alisema wanachama "wengi" wa Sinodi Kuu "wamepuuza" wasiwasi wake kuhusu mageuzi ya hivi majuzi.

Chanzo: Bbc