Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waadventista Wasabato wataka amani idumishwe

11722 WASABATO+PIC TanzaniaWeb

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato Segerea na Bonyokwa jijini Dar es salaam wamefanya maombi ya kudumisha amani ya Taifa, kupitia sikukuu maalumu ya vibanda kwa kanisa hilo duniani. 

Sikukuu hiyo hufanyika kila mwaka kwa waumini hao hapa nchini na duniani kote kupitia utaratibu wa kukutana pamoja na kuabudu kwa siku kadhaa katika makambi maalumu, ambapo hapa nchini huanza Julai hadi Novemba.

Kambi la waumini hao zaidi ya 1,200 kwa mtaa wa Segerea walianza kukutana hivi karibuni wakiwa na kauli mbiu ya "Mungu kwanza" kabla ya kuamua au kufanya jambo lolote katika maisha ya Mtanzania.

Akizungumza wakati wa kilele cha kambi hiyo, Kiongozi wa baraza la wazee wa kanisa la wadventista wa sabato, Cleopa Mwaitete alisema kauli mbiu ya "Mungu kwanza" inawataka Watanzania kujisalimisha nafsi zao mbele ya Mungu ili aweze kuwa msaada wa changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa maadili.

"Dunia inazidisha changamoto, matumizi ya mitandao, watoto wetu wanaharibika kimaadili, kwa hiyo tukimtanguliza Mungu ndiyo salama ya Taifa na jamii zetu. Katika makambi haya tunafuatikia maisha ya vijana wetu kuanzia kanisani hadi huko mtaani na nyumbani, "alisema Mwaitete.

Alisema maombi hayo yatasaidia kuokoa jamii inayoshambuliwa na changamoto za matumizi ya dawa za kulevya, rushwa, watu kukosa uaminifu na wazazi wengi walioshindwa kutimiza majukumu yao kwa familia.

Mchungaji wa Jimbo dogo la Segerea, Kibunto Daniel alisema tangu walipokutana katika kambi hiyo, wameshiriki ibaada ya kumshukuru Mungu, mafunzo ya wanandoa, warsha za vijana na maisha huku Mchungaji na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arusha, Paul Semba akiongoza kilele cha makusanyo hayo.

Kwa mujibu wa Mchungaji Kibunto, zaidi ya makambi 10 yanaendelea katika jiji la Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano wa makambi mtaa wa Segerea, Albert Chamriho alisema Taifa na kila Mtanzania anamuhitaji Mungu wakati wowote kabla ya kuanza jambo lolote.

Alisema makambi hayo yamekuwa msaada wa jamii hususani vijana katika kukabiliana na changamoto ya kimaadili na kuacha vitendo vya uharifu.

Chanzo: mwananchi.co.tz