Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini wazindua kitabu cha uchumi wa soko jamii Tanzania

66550 Pic+dini

Fri, 12 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dae es Salaam. Viongozi wa dini wamezindua kitabu cha Uchumi wa Soko Jamii kwa Tanzania kitakachosaidia Taifa kuelekea kwenye mkakati wa uchumi wa viwanda bila kumwacha mtu yeyote nyuma.

Kitabu hicho kilichozinduliwa leo Ijumaa Julai 12, 2019 kimeandikwa kwa ushirikiano wa  Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Akizindua kitabu hicho mwenyekiti wa umoja wa viongozi wa dini Tanzania, Askofu Steven Munga amesema kabla ya kuandika, baadhi ya wasomi walienda nchi mbalimbali duniani kufanya utafiti kuhusu uchumi wa soko jamii usiomwacha yeyote nyuma.

Askofu Munga amesema uchumi huo ni ule ulio katika mfumo chotara  unaounganisha ujamaa na ubepari.

"Mfumo huu ni fursa ya kuibadilisha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi imara, shirikishi na yenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii," amesema Askofu Munga.

Alli Muhidini Mkoyogole, mwakilishi wa Mufti  wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir, amesema kitabu hicho kitawasaidia waumini kujiimarisha kiuchumi.

Pia Soma

Kwa upande wake Shekh wa Mkoa wa Mwanza,  Hassan Kabeke  amesema watakitumia kuwajenga waumini wao kiuchumi.

"Kila kiongozi wa dini anao wajibu wa kufundisha watu wake kujitafutia riziki na kujiimarisha kiuchumi, Uislamu pia umeelekeza habari za uchumi hata Quran inatuelekeza fanyeni kazi," amesema Shekh Hassan.

Mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) aliyesaidia kuandika kitabu hicho,  Ponsian Ntui amesema kukiwa na jamii iliyoelimika uchumi wa nchi unaweza kukua kwa kasi.

Chanzo: mwananchi.co.tz