Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini, wazee wataka uchaguzi wa Amani

1d2f9c3f9c5e461fd9078c5b4b4537f6 Viongozi wa dini, wazee wataka uchaguzi wa Amani

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na wazee maarufu mkoani Simiyu wamekutana kujadili mwenendo wa amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu.

Viongozi hao wakiongozwa na Mchungaji Martin Nketo wamekutana jana wakiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kupiga kura kwa amani Oktoba 28 mwaka huu.

Walisema jamii nzima ina wajibu wa kuilinda na kuitunza amani kabla na baada ya uchaguzi.

Akisisitiza umuhimu wa kuituza amani ambayo ni ngumu kuirejesha iwepo ikipotea mzee Sule Kija alisema amani imeasisiwa tangu wasisi wa nchi hii walipo pigania uhuru hivyo ni wakati wa kupambana kuilinda.

"Waasisi na viongozi wote waliotawala wametuachia amani hivyo basi tunatakiwa tupambane kuhakikisha amani hii haipotei,"Kija

Walisema kuwa waumini ni miongoni mwa wapiga kura ambao wanatakiwa kuhamasishwa amani kwani wao ndio wenye jukumu kubwa la kuhubiri amani katika nyumba za ibada ili ujumbe uwafikie kwa urahisi zaidi.

Nae Mchungaji Joseph Abel alisema kuwa wakati uliobaki ni ni wa kuwashauri waumini kuweza kujua kuwa wao ni ngao ya amani na wanawajibu wa kulinda amani hiyo.

"Haya makundi yalipo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi inabidi yatendewe haki, kwa sababu haki ndio msingi wa amani haki ikitendeka amani itasalia amani inaambatana na haki," alisema Mchungaji Joseph.

Akitilia mkazo wa kutenda haki bila kujali itikadi za kidini kwa waumini mchungaji Samwel Matwiga alisema hakuna maana ya matamko yasiyokuwa na tija kwa Taifa kwa sababu yanalenga kuwagawa waumini na kuvuruga dhima ya watumishi kuwa wajenzi wa amani.

Kikao hicho kilimalozika kwa maazimio manne ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kupiga kura, wananchi kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na tume ya uchaguzi kwa wapiga kura.

Chanzo: habarileo.co.tz